Everton Yakamilisha Usajili wa Mykolenko.

Klabu ya Everton imefanikiwa kukamilisha usajili miaka minne na nusu wa beki wa kushoto wa Ukraine, Vitaliy Mykolenko akitokea klabu ya Dynamo Kyiev.

 

Mykolenko, 22 amejiunga na Everton kwa dau ambalo halijawekwa wazi akiwa amefanikiwa kucheza mechi 21 katika timu ya taifa atachukua nafasi ya Lucas
Digne ambaye amekuwa akiandamwa na majeraha.

Mchezaji huyo anakuwa ni usajili wa sita kwa meneja Rafael Benitez tangu ajiunge Goodison Park. Mykolenko anaimani ataweza kupambana katika ligi ya EPL.

“Mpira umezaliwa katika ligi ya EPL na natumaini ligi hii itaendana na uchezaji wangu.” alisema.

“Nina miaka 22 sijihisi kama mtoto tena. Nina uzoefu kucheza kwenye ligi za ulaya na natumaini nitaendelea kujiboresha kama mchezaji.

“Nina furaha kupata nafasi ya kucheza mbele ya mashabiki zetu wa Everton. Nimeona mechi kadhaa hapa Goodison Park na walikuwa wanashangaza.” aliongeza.


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.