Kocha msaidizi wa Yanga SC, Cedrack Kaze, amekiri kuwa wapinzani wao Azam FC walistahili ushindi walioupata baada ya kucheza vizuri ndani ya dakika 90 kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo juzi jioni.

Kaze akizungumza alisema kwenye mchezo huo wa juzi wapinzani wao walikuwa vizuri zaidi eneo la katikati ambalo liliwasaidia sana kumiliki mpira.
“Tumekubali kuwa tumetolewa, nawapongeza sana Azam walikuwa vizuri sana eneo la katikati la uwanja na walicheza vizuri kwa ujumla na walistahili kusonga mbele,” alisema Kaze.
Kaze pia alitoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kumtoa golikipa aliyecheza kwa karibu dakika zote za mchezo huo Aboutwalib Mshery na kuingia Erick Johora zikiwa zimebaki dakika za nyongeza.
Kocha huyo alisema mabadiliko hayo yalikuwa ya kawaida na ya kiufundi kutokana na alichokiona mazoezini kwenye mazoezi ya mikwaju ya penati.
“Ni mabadiliko ya kawaida tu, Johara alifanya vizuri sana kwenye mazoezi, tulifanya mazoezi ya penalti na akaonekana kuwa vizuri ndio msingi wa mabadiliko yale,” aliongeza.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

