Kompany Amtaka Pep Kukataa Kumhusisha na Kazi City

Kocha wa Burnley Vincent Kompany amemtaka Pep Guardiola kuacha kuzungumza naye kama kocha wa baadaye wa Manchester City wakati bado yuko katika hatua za awali za kazi yake ya ukocha.

 

Gwiji wa City Kompany, ambaye alishinda tuzo kuu 10 katika kipindi cha miaka 11 katika Uwanja wa Etihad, atamenyana na timu yake ya zamani katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA leo hii.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Kompany kurejea uwanjani, ambapo sanamu ya kuheshimu wakati wake katika klabu hiyo iliwekwa mnamo Agosti 2021, katika kile kinachotarajiwa kuwa muungano wa hisia.

Baada ya misimu miwili kuifundisha Anderlecht, Kompany amepata mafanikio makubwa katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha wa Burnley, ambao wanapania kupandishwa daraja kutoka msimu ukimalizika.

Kompany amesema kuwa Guardiola aache kumtazama kama mrithi wa baadae hapo City yeye ni kocha wa michuano hajui anataka nini kwake, na anadhani kuwa Pep anapswa kusalia kwa miaka 10 zaidi Manchester City kwanza kwani klabu hiyo inashindania kushinda ubingwa na hadhani kama mazungumzo ya aina hiyo hayana maana.

Miongoni mwa pongezi zingine, Guardiola alimsifu Kompany ambaye alifanya naye kazi kwa misimu mitatu  kwa kuanzisha mtindo wa kipekee wa kucheza huko Burnley haraka sana.

Alipoulizwa kama maoni ya Guardiola yanaongeza shinikizo kwenye kazi yake ya ukocha, Kompany alisema: “Shinikizo ni jambo la akili yako mwenyewe. Nadhani ukicheza fainali kubwa uko sawa na shinikizo, lakini najaribu kuwa na busara kadri niwezavyo. Niko katika mazingira ambayo watu ninaofanya nao kazi wana busara ya kutosha kutofanya kazi yangu kutegemea ikiwa tutaifunga Manchester City.”

Nilikuja Burnley kwa sababu niliichagua kwa ajili ya watu. Ni mazingira ambayo nina nafasi ya kujifunza na kuwa bora. Alisema kocha huyo.

Burnley hawajashinda ugenini wakiwa na City tangu 1973 Ngao ya Hisani, sare nne na kupoteza mechi 12 kati ya 16 walizotembelea tangu wakati huo.

Acha ujumbe