Onyango Aandika Barua TFF

Mchezaji wa klabu ya Simba Joash Onyango ambaye anacheza katika nafasi ya beki wa kati ameiandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kutaka timu hiyo ivunje mkataba wake na Simba kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimeelzwa.

 

Onyango Aandika Barua TFF

Onyango anadai kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona kuwa hana nafasi ya kucheza katika kikosi Simba  kutokana na ujio wa Mohamed Outtara ambaye amekuwa ni chaguo la kwanza la mwalimu Zoran Maki mpaka sasa.

Toka ligi ianze msimu huu Onyango hajapata nafasi hata moja ya kuanza kwenye timu hiyo hata kuingia katika wachezaji wa akiba hivyo anataka atimke kunako klabu nyingine ili akatafute changamoto mpya sehemu nyingine.

Onyango Aandika Barua TFF

Joash Onyango ambaye ni raia wa Kenya alisajiliwa na Simba mwaka 2020 kuja kuitumikia klabu hiyo ambapo alitokea katika klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya. Beki huyo amepata mafanikio na Simba ambapo ameweza kuchukua kombe la ligi kuu, Kombe la Azam Sports Federation, Mapinduzi na mengine mengi, Vilevile na kufika robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani Africa na Shirikisho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.