Klabu ya Azam FC yaendeleza wimbi la ushindi hapo jana walipokuwa wageni wa Namungo ya Lindi baada ya kuitwanga kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa majira ya saa 1:00 jioni katika uwanja wa Majaliwa.

 

Azam FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi

Dakika ya 29 tu Azam ilikuwa imeshajipatia bao kupitia kwa beki wao Edward Manyama na ndilo bao ambalo lilisalia mpaka kumalizika kwa mchezo huo huku Namungo wakipoteza mchezo wao wa tatu mfululizo.

Azam FC ya ambayo ipo chini ya Kally Ongala inaendeleza makali yake ya kujipatia ushindi mnono kwa kila mechi ambazo inakabiliana nazo huku ikiwa ni mechi ya sita kushinda.

Azam FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi

Namungo walipata adhabu ya kadi nyekundu kipindi cha pili na na kufanya kucheza wakiwa pungufu huku wakijaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini milango ikawa migumu huku mlinda mlango wa Wanalamba lamba akiwa na ubora wa hali ya juu.

Baada ya ushindi huo matajiri hao wa Chamazi wakipaa hadi kileleni wakipanda hadi nfasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zao 29 huku Namungo wao wakisalia katika nafasi ya 8 baada ya kupoteza.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa