Azam Yachapika Nyumbani Kwake

 Ligi kuu ya NBC iliendelea hapo jana kwa michezo mitatu ambapo mchezo wa mwisho ulikuwa ni kati ya Azam FC dhidi ya Namungo fc na kuisha kwa Matajiri wa Chamazi kupoteza mchezo huo.

 

Azam Yachapika Nyumbani Kwake

Azam ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 19 ambalo lilikuwa bao la kujifunga kabla ya baadaye Kabunda na Kichuya kupachika mabao mawili ya ushindi na kuondoka na pointi tatu.

Baada ya kupoteza mchezo huo Azam wameendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 53 baada ya kucheza michezo 28 kwenye ligi huku Namungo wao wapo nafasi ya 5.

Mechi ijayo ya Wanalamba lamba watasafiri hadi Mkwakwani Tanga kukiwasha dhidi ya Coastal Union ambaye yeye yupo nafasi ya 10 baada ya kushinda mechi ya jana huku ushindi pekee ndio utakaomuweka kwenye nafasi nzuri.

Azam Yachapika Nyumbani Kwake

Wakati Namungo yeye atamkaribisha Dodoma Jiji ambaye ametoka kupoteza dhidi ya Mabingwa wa ligi Yanga. Hivyo nae pia pointi tatu zitakuwa ni muhimu kwake kama anataka kusalia kwenye ligi.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.