Baada ya kupoteza mechi iliyopita timu ya Dodoma Jiji kesho wanashuka Dimbani kukiwasha dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Jamhuri, mchezo utakaopigwa saa 2: 15 usiku.

Dodoma jiji hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye Ligi kwani mpaka sasa wamejivunia alama 18 pekee kwenye michezo waliyocheza, wakishinda mechi zao 5 pekee, sare 3 na kupoteza mara 10.
Kagera Sugar ya Mexime wao wamekusanya jumla ya pointi 24, wakishinda michezo 6, sare 6, kupoteza mara 6 pia na pia kwenye msimamo wapo nafasi ya 6. Pia timu hii kutoka Kaitaba wametoa sare mechi 3 mfululizo.
Wakati Walima Zabibu wao wakiwakipoteza mech mbili mfululizo na wakihitaji alama tatu kesho kwa hali na mali ili waepuke kushuka daraja msimu huu kwani kwasasa wana kocha mpya.

Mechi mbili za mwisho walizokutana kwenye Ligi kulikuwa hakuna mbabe, hivyo kesho mechi ya tatu nani atakuwa mbabe na kuondoka na pointi tatu?

