Mchezaji mpya wa klabu ya Simba Saidoo Ntibazonkiza inasemekana anaweza kuwepo kwenye mchezo wa klabu ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Ijumaa.
Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa kutoka klabu ya Geita Gold kwenye dirisha dogo la usajili siku kadhaa zilizopita, Inaelezwa anaweza kucheza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC siku ya ijumaa.
Saidoo Ntibazonkiza amekua na kiwango bora sana ndani ya Geita baada ya kuhusika kwenye mabao kumi ya ligi kuu, Akifanikiwa kupiga pasi sita za mabao na kufunga mabao manne ikiwa ni miongoni mwa mambo yaliyoivutia klabu ya soka ya Simba.
Klabu ya Simba inapambana kupata kibali cha kazi cha mchezaji huyo na kama mambo yatakwenda sawa basi mchezaji huyo atavaa uzi wa klabu ya Simba siku ya kesho kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Prisons.
Mchezaji Saidoo Ntibazonkiza raia wa Burundi pia anatarajiwa kua miongoni mwa wachezaji ambao watasafiri na klabu hiyo kuelekea visiwani Zanzibar kwajili ya michuano ya kombe la mapinduzi ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku kadhaa zijazo.

