Kiungo wa zamani vilabu vya Yanga na Geita Gold Saidoo Ntibazonkiza amejiunga na klabu ya Soka ya Simba kwa mkataba mwaka mmoja na nusu kuwatumikia wekundu wa msimbazi.
Kiungo huyo raia wa Burundi amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Geita Gold akiwa na namba nzuri kuliko mchezaji yeyote ndani ya klabu hiyo, Mcxhezaji huyo ambaye mpaka sasq qmehusika kwenye magoli kumi ya klabu hiyo kwenye ligi kuu huku akifanikiwa kufunga mabao manne na pasi sita za mabao.
Klabu ya Simba imekamilisha dili hilo huku ikiwa na uhakika sasa kua na mbadala wa mchezaji wao nyota kikosini Clatous Chama, Simba wamemsajili Ntibazonkiza kwajili kuongeza ubora kwenye kikosi chao lakini pia kuziba pengo la Chama pale anapokua anakosekana.
Wekundu wa Msimbazi wamefanikiwa kufungua dirisha dogo la usajili kwa staili ya aina yake baada ya kumsajili kiungo huyo matata, Huku mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo Salim Abdallah Try Again akisema kazi imeanza na mazuri zaidi yanakuja.
Kiungo Saidoo Ntibazonkiza kwa taarifa za ndani zinaeleza mchezaji huyo ameonekana mkoani Mwanza mapema leo akiwa na Afisa habari wa timu ya Simba, Ikumbukwe klabu ya Simba itacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC kwenye dimba la CCM Kirumba siku ya jumatatu.

