Singida Big Stars Kumkaribisha Geita Gold Kesho

Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara kuendelea kesho kwa michezo mitatu ambapo kati ya hiyo michezo, mchezo wa mapema ni kati ya Singida Big Stars dhidi ya Geita Gold majira ya saa 10:00 Jioni.

 

Singida Big Stars Kumkaribisha Geita Gold Kesho

Mchezo wa Singida utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo vijana hao wa Hans wakiwa wametoka kuchukua pointi tatu mchezo uliopita kwa Walima Zabibu kwa bao pekee la Gomes.

Kesho ni zamu ya Wachimba Dhahabu ambao wao wametoka kutoa sare ya pili mfululizo huku wakihitaji pointi tatu muhimu zitakazowawezesha kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Singida wapo nafasi ya 4 baada ya kushinda mechi zao 10, sare 4, na kupoteza mara 4 wakiwa na pointi zao 34 huku ushindi wa hapo kesho utawafanya wafikishe pointi 37 zitakazowaweka kwenye nafasi ya 3.

Singida Big Stars Kumkaribisha Geita Gold Kesho

Vijana wa Minziro wapo wapo nafasi ya 7 kwenye ligi,wakiwa wameshinda mechi zao 5, sare 9 na kupoteza mara 4, pointi 24 kibindoni. Tofauti yao ni pointi 10 hadi sasa. Nani kuibuka na pointi tatu zote kesho?

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.