Singida Big Stars Yachukua Pointi 3 kwa Dodoma Jiji

Timu ya Singida Big Stars imeondoka na pointi 3 zote katika mchezo wao wa jana waliokuwa wakimenyana dhidi ya Dodoma Jiji katika uwanja wa Jamhuri majira ya saa 1:00 usiku.

 

Singida Big Stars Yachukua Pointi 3 kwa Dodoma Jiji

Singida wamepata pointi hizo tatu baada ya kushinda bao 1-0 ambalo lilifungwa katika dakika ya 80 na Bruno Gomes huku dakika 90 za mwamuzi zikikamilika na vijana hao wa Hans wakiondoka kifua mbele.

Baada ya ushindi huo Walima alizeti sasa wamefikisha pointi zao 34, wakiwa nafasi yao ile ile ya 4, huku wakiwa nyuma ya pointi nne kwa anayeshikilia nafasi ya tatu na pointi 13 kwa aliyepo kileleni.

Singida Big Stars Yachukua Pointi 3 kwa Dodoma Jiji

Dodoma Jiji wao wapo nafasi ya 12 baada ya kupoteza mchezo wa pili mfululizo na mchezo unaofuata wanatarajia kumkaribisha Kagera Sugar siku ya Ijumaa ambye ametoka kutoa sare.

Wakati kwa vijana wa Hans wao watakiwasha dhidi ya Geita Gold katika uwanja wao wa Liti huko Singida.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.