Singida Big Stars Kuwafuata Dodoma Jiji Kesho

Klabu ya Singida Big Stars baada ya kutoa sare ya Mbeya City watakuwa ugenini hapo kesho kuzichapa dhidi ya Dodoma Jiji majira ya 2:15 usiku katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

 

Singida Big Stars Kuwafuata Dodoma Jiji Kesho

Singida wameanza msimu huu vizuri toka wapande ligi kuu kwani mpaka sasa wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa wamejikusanyia pointi zao 31 baada ya kushinda mechi zao 9 sare nne na kupoteza mara 4.

Wakati wenyeji wao Dodoma bao wanajikongoja kupanda nafasi za juu ambapo wapo nafasi ya 12 baada ya kupoteza mchezo uliopita, huku wakiwa hawana mwendelezo mzuri wa matokeo.

Singida Big Stars Kuwafuata Dodoma Jiji Kesho

Wameshinda michezo mitano pekee kati ya 17 waliyoshuka dimbani, wakienda sare mara tatu, kupoteza mara tisa na kujivunia alama 18 ambazo bado sio salama mpaka sasa kama wanataka kubakia kwenye Ligi msimu ujao.

Mechi ya kwanza kukutana walitoa suluhu. Je hapo kesho nani kuibuka kidedea na kuondoka na pointi zote 3?

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.