Geita Gold Kusaka pointi 3 Nyumbani

Klabu ya Geita Gold inatarajia kumkaribisha Dodoma Jiji nyumbani kwake kusaka pointi tatu ambazo amezikosa kwa muda mrefu majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Nyankumbu.

 

Geita Gold Kusaka pointi 3 Nyumbani

Geita Gold ambayo imeekuwa ikipata matokeo mabaya kutokana na kupoteza baadhi ya wachezaji wao bora waliokuwa nao akiwemo Saido Ntibanzokiza, Yusuf Kagoma, Nashon na wengine wengi lakini haijatafuta wengine hali ni mbaya.

Katika michezo mitano iliyopita ametoa sare tatu na kapoteza michezo miwili akishikilia nafasi ya 8 akiwa na pointi zake 24.

Wakati Dodoma Jiji wao wametoka kumtambulisha aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Namungo Steven Sey wakitarajia anaweza akawasaidia katika eneo la ufungaji, huku michezo yao mitano ya nyumba wameshinda mitatu na kupoteza miwili.

Geita Gold Kusaka pointi 3 Nyumbani

Dodoma wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama zao 21, na ushindi wa leo utawapelea hadi nafasi ya nane.

Mechi ya mwisho kumenyana Walima Zabibu waliondoka na pointi tatu wakiwa nyumbani kwao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.