Ihefu Kujiuliza Kesho Dhidi ya Mtibwa Sugar

Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara kuendelea kesho ambapo timu ya Ihefu itakuwa nyumbani kumkaribisha Mtibwa kutoka Morogoro.

 

Ihefu Kujiuliza Kesho Dhidi ya Mtibwa Sugar

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 8:00 mchana katika uwanja wa Mbarali huku Ihefu wakihitaji pointi tatu hizo kwa hali na mali ili waendelee kusalia katika ligi kwani bado wana hali mbaya.

Ihefu wapo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi kuu wakiwa wameshinda mechi zao nne kati ya 17 walizocheza, sare mbili na kupoteza michezo 11 hadi sasa wakiwa wamejikusanyia pointi 14 kileleni.

Ihefu Kujiuliza Kesho Dhidi ya Mtibwa Sugar

Wakati kwa upande wa Mtibwa Sugar wao wapo nafasi ya 5 ambayo ni nafasi nzuri, michezo 17 waliyocheza wameshinda sita, sare sita, na wamepoteza michezo mitano wakijikusanyia alama 24 kibindoni.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, Mtibwa aliibuka mshindi na kuondoka na alama zote tatu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.