Baada ya kupata pointi 3 muhimu mchezo wake uliopita, leo hii Ihefu atakuwa mgeni wa Namungo katika mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC utakaopigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa Majaliwa.

 

Ihefu Ugenini Leo Dhidi ya Namungo

Ihefu wapo nafasi ya 14 kwenye Ligi, wakiwa na pointi zao 14, mechi 16 wameshinda nne, sare mbili na kupoteza 10, wakiwa wameanza kujikongoja kutoka mkiani hadi sasa wapofikia.

Namungo yeye ametoka kutoa sare mchezo wake uliopita akitarajia kupata ushindi mchezo wa leo ili aweze kusogea hadi nafasi ya nane akishinda mchezo wa nyumbani hii leo.

Namungo ameshinda mechi zake tano, ameenda sare mara nne na kupoteza mara saba akijivunia pointi 19.

Ihefu Ugenini Leo Dhidi ya Namungo

Ihefu ya Katwila wao wanahitaji ushindi kwa namna yoyote kwani nafasi waliyopo bado haiwahakikishii kusalia ligi kuu msimu ujao.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa