Mtama Waliwa na Ihefu

Katika mwendelezo wa Kombe la Shirikisho la Azam klabu ya Ihefu imeitungua timu ya Mtama Boys kwa mabao 9-0 hapo jana katika uwanja wa Highlands Estate na kusonga mbele kwenye michuano hii.

 

Mtama Waliwa na Ihefu

Mabao hayo yalitupiwa kimyani katika vipindi vyote vya mchezo ambapo kufikia dakika 45 za kwanza za mchezo Mtama alikuwa tayari ameshafungwa mabao 8-0 kitu ambacho ilikuwa ni mzigo kwake.

Mtama Boys wanacheza Ligi daraja la tatu hivyo haikuwa kwake kucheza na timu ya Ligi kuu Ihefu ambayo nayo kwenye ligi mambo bado magumu kutokana na matokeo ambayo wanayapata.

Mtama Waliwa na Ihefu

Mabao ya Ihefu yalifungwa na Ngoah Willy, na Sinchimba akatupia mabao yake 5 ya kutosha na kukamilisha jumla ya idadi ya mabao 9, halafu akapewa mpira wake kwa Hat-trick zake.

Acha ujumbe