Je Polisi Tanzania Kuendelea Kushikilia Mkia Hapo Kesho?

Baada ya timu ya Polisi Tanzania kupoteza mchezo wao uliopitwa wakiwa nyumbani, hapo kesho wanatarajia kumualika Azam FC kwenye mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

 

Je Polisi Tanzania Kuendelea Kushikilia Mkia Hapo Kesho?

Polisi ambao wanashikilia nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi, wanatarajia kupata ushindi mechi ya kesho kwa Wanalamba lamba ambao wameenda mechi saba huku wakiwa wameshinda mechi zote nao wakizisaka hizo pointi 3.

Ikumbukwe kuwa timu hiyo ya maafande wametoka kumtambulisha aliyekuwa kocha wa zamani Mwinyi Zahera kuwa kama kocha wao mkuu wa kukinoa kikosi hicho huku mkataba huo ukiwa ni wa miezi sita pekee.

Je Polisi Tanzania Kuendelea Kushikilia Mkia Hapo Kesho?

Lakini pia toka Kally Ongala akabidhiwe matajiri hao wa Chamazi ameipatia ushindi pekee timu hiyo huku kesho itakuwa mechi yake ya nane toka achukue timu hiyo. Je Zahera atafanya nini hapo kesho na Polisi?

 

 

Acha ujumbe