Ben White Hatosafiri na Arsenal Kufuatia Kujiondoa Kwenye Kombe la Dunia

Beki wa Arsenal Ben White hatasafiri na klabu yake ya The Gunners kwenda Dubai Jumapili kufuatia kujiondoa kwenye kikosi cha Uingereza.

 

ben white

White alirejea nyumbani akitokea kwenye kambi ya timu ya Uingereza inayoendelea kujifua kuelekea mechi yao ya leo ya hatua ya 16 bora dhidi ya Senegal kutokana na sababu binafsi.

Kama ilivyoripotiwa na ESPN, Ben White hatakuwa miongoni mwa kundi la kwanza la wasafiri kwenye kikosi cha Arsenal kwenda Dubai Jumapili na haijulikani kama atajiunga nao siku ya baadaye.

Vinara hao wa EPL wanatazamiwa kushiriki Kombe la Dubai Super Cup wakati wa mapumziko ya Kombe la Dunia dhidi ya Lyon Alhamisi na AC Milan mnamo Desemba 13.

Mikel Arteta anatumia kambi ya mazoezi yenye hali ya hewa ya joto huko Dubai kurudisha kikosi katika hali nzuri kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu.

 

ben white

FA katika taarifa yake imethibitisha kuwa beki huyo ambaye bado hajachezea timu ya Three Lions ameondoka kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Al Wakhrah na kwamba haikutarajiwa angerejea Qatar.

“Ben White ameondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Uingereza huko Al Wakrah na kurejea nyumbani kwa sababu za kibinafsi,”

“Beki wa Arsenal hatarajiwi kurejea kikosini kwa muda uliosalia wa michuano hiyo. Tunaomba kwamba faragha ya mchezaji iheshimiwe kwa wakati huu.” ilisema taarifa hiyo.

 

ben white

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe