Kapombe na Mohamed Hussein Waongezwa Timu ya Taifa

Baada ya timu ya Tanzania Taifa Stars kurejea nchini, wakitokea Uganda walipokuwa wakicheza mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon, Kocha mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche amewaita Kapombe na Zimbwe kujiunga kambini.

 

Kapombe na Mohamed Hussein Waongezwa Timu ya Taifa

Kikosi kilivyotoka kwa mara ya kwanza na mabeki hawa wa Simba wanaocheza pembeni kukosekana Kapombe na Muhamed Husssein maneno yalikuwa ni mengi sana hasa kutokana na viwango vyao.

Lakini baada ya kocha wa Stars Adel kuwashuhudia mabeki hawa tegemezi kabisa wa Simba wakicheza kwenye mchezo dhidi ya Horoya ambao mnyama aliibuka na mabao 7-0, alishangaa kwanini hawakuitwa kwenye timu.

Lakini pia baada ya mchezo ule wa Simba kumalizika dhidi ya Horoya picha mbalimbali zilisambaa zikiwaonyesha Shomari Kapombe na Zimbwe wakiwa wanateta kitu na kocha huyo wa timu ya Taifa na wengei wakisema kuwa anawataka haraka sana kwenye timu.

Kapombe na Mohamed Hussein Waongezwa Timu ya Taifa

Timu ilienda Uganda na ikashinda bao 1-0 la Simon Msuva na ipo nafasi ya pili kwenye kundi, na mechi ya marudiano itapigwa siku ya Jumanne katika dimba la Benjamin Mkapa na leo hii tayari mabeki hao wameshajiunga na wenzao kambini kwaajili ya mchezo huo unaofuta.

Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa mwalimu huyo mpya wa Taifa Stars sio kwamba alikuwa haijui timu alivyoiita bali alikuwa anaifatilia na wachezaji alikuwa anawaangali kwenye timu zao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.