Rais wa klabu ya Fc Barcelona Joan Laporta amesema milango iko wazi kwa Lionel Messi kurejea ndani ya klabu hiyo huku akiahidi kuboresha mahusiano baina ya mchezaji huyo na klabu ya Barcelona.
Rais Laporta amekua akionesha mapenzi yake kwa Lionel Messi mara kwa mara anapohojiwa na waandishi wa habari, Vilevile amekua akitoa fursa kwa mchezaji huyo kurejea ndani ya miamba hiyo soka nchini Hispania ambayo imempa umaarufu mkubwa mchezaji huyo.
Lionel Messi anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu ndani ya klabu yake ya sasa ya PSG, huku vyombo mbalimbali vikieleza nyota huyo anaweza kurejea ndani ya klabu ya Barcelona lakini vilevile uwezekano wa kusalia ndani ya PSG upo kwakua mazungumzo bado yanaendelea.
Laporta anasema yupo kwenye mchakato wa kuhakikisha anatengeneza mahusiano mazuri baina ya klabu ya Barcelona na Lionel Messi, Hali ambayo imeibua maswali mengi na wengi kuwaza moja kwa moja kua Rais huyo anataka kumalizana na mchezaji huyo ili arudi kwenye viunga vya Camp Nou.
Upande mwingine Rais wa klabu ya PSG Nasser Al- Khelafi amesema yuko kwenye mchakato wa kuhakikisha Lionel Messi, Mbappe, Ramos wanasalia ndani ya klabu ya PSG hivo mpaka sasa inaonekana vita inapamba moto baina ya pande mbili kwani Barcelona wanataka kumrudisha huku PSG wanataka kumbakiza staa huyo.

