Kapombe Arejea Kikosi cha Kwanza Simba

Beki wa kulia wa klabu ya Simba Shomari Kapombe amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Simba baada ya kua nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake.

Mchezaji huyo mwandamizi ndani ya kikosi cha Simba ameonekana kwenye kikosi cha kwanza klabu hiyo kitakachomenyana na klabu ya Mtibwa Sugar katika dimba la Benjamin Mkapa mida ya saa moja kamili usiku.kapombeShomari Kapombe alieitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa kurejea kwake kumekua sehemu ya faraja kwa mwalimu wa klabu hiyo Juma Mgunda, Lakini pia mashabiki wa klabu hiyo ambao waliamini kukosekana kwa beki huyo ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc.

Beki Shomari Kapombe amerejea kwenye kikosi moja kwa moja lakini pia pia anarudi na wachezaji wengine muhimu kwenye timu hiyo kama Sadio Kanoute, Pamoja Mzamiru Yassin ambao walikosekana michezo iliyopita.kapombeBeki huyo ambae nafasi yake ilikua ikichezwa vizuri na Israel Mwenda ambae na yeye amepata majeraha kitu kilichomfanya beki Shomari kurejea moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.