Kabla ya mechi yao dhidi ya Nottingham Forest, wachezaji wa Arsenal walituma ujumbe wa kumuunga mkono Pablo Mari ambaye ni mlinzi wa Monza kwa sasa akiwa klabuni hapo kwa mkopo ambaye alifanyiwa upasuaji baada ya kuchomwa kisu huko Italia.
Lakini pia wameweza kumuunga mkono baada ya kufunga bao lao la kwanza kwenye mchezo huo ambao unaendelea huku wakimtaka mchezaji huyo apone kwa haraka ili aweze kurejea uwanjani.
Kikosi hicho kilipiga picha na jezi ya Pablo Mari ya Arsenal wakati wa kujiandaa na Uwanja wa Emirates. Tukio hilo lilitokea Assago, viungani mwa Milan, katika kituo cha biashara siku ya Alhamisi jioni.
Pablo Mari aliripotiwa kuwa wa kwanza kuchomwa kisu mgongoni na alifanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa asubuhi kusaidia kushona baadhi ya misuli ya mgongo iliyokuwa imeharibika.
Pablo Mari ameambiwa apumzike kabisa na hatarajiwi kurejea uwanjani kwa muda wa miezi mitatu ili kuangalia afya yake inaendeleaje huku mchezaji huyo akitumia msimu huo kuwa kwa mkopo Mozna.