Mamadou Doumbia wa Yanga Afiwa na Baba Yake Mzazi

Mamadou Doumbia ambaye ni usajili mpya wa Yanga ambao wameufanay dirisha dogo la usajili juu ya mchezaji huyu, ameripotiwa kuwa amefiwa na baba yake mzazi.

 

Mamadou Doumbia wa Yanga Afiwa na Baba Yake Mzazi

Kifo hicho cha baba mzazi wa Mamadou kimeripotiwa jana April 13, 2023 nchini Mali na hivyo mchezaji huyo anatarajia kusafiri mapema leo hii kwenda Mali kwaajili ya kushiriki mazishi ya baba yake.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa wananchi, wametoa salamu za pole kufuatia msiba huo na wanatoa pole kwa wanafamilia katika kipindi hiki kigumu ambacho wanapitia kwasasa baada ya kuondokewa na mpendwa wao.

Mamadou Doumbia wa Yanga Afiwa na Baba Yake Mzazi

Mamadou toka asajiliwe na Yanga amekuwa hapati nafasi mara kwa mara za kwenye nafasi ya beki kutokana na ushindani uliopo kwenye eneo hilo lakini pia sio chaguo nambari moja kwa kocha Nabi.

Klabu hiyo inatarajia kushuka dimbani wikendi hii kukiwasha dhidi ya mtani wake Simba kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu ya NBC huku mechi ya mwisho kukutana walitoshana nguvu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.