MAXI NZENGELI STAA MPYA YANGA

Nyota Maxi Nzengeli ndani ya kikosi cha Yanga ni ngoma nzito kutokana na uwezo wake wa kufunga na kutengeneza nafasi kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.

 

MAXI NZENGELI STAA MPYA YANGA

Nzengeli anayevaa uzi namba 7 mgongoni huku mtindo wake unaomtambulisha ukiwa ni ule wa kuchomekaa jezi rekodi zinaonyesha kuwa bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Yanga alipachika dakika ya 7.

Kahusika kwenye mabao matano ya kufunga, akiwa ametoa asisti moja dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kutupia mabao manne.

Mabao mawili ya Maxi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa dhidi ya ASAS FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na mabao mawili ndani ya ligi mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

MAXI NZENGELI STAA MPYA YANGA

Maxi ana spidi, maamuzi ya haraka na pasi ndefu ikiwa ni nguzo yake kubwa akiwa uwanjani huku mguu wake wenye nguvu ukiwa ni ule wa kulia.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania alipiga pasi ndefu zaidi ya sita ambazo zilifika wa wahusika na kwenye mchezo wa ligi dhidi ya ASAS FC pia alipiga pasi ndefu zaidi ya saba zilizofika kwa walengwa.

Uwezo wake wa maamuzi ya haraka na spidi unathibitishwa na pasi zake anazotoa kwa kuwa ni mchezaji asiyependa kukaa muda mrefu na mpira akipewa pasi anaiongezea mwendo jambo linalomfanya awe anapewa nafasi na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameliambia Spoti Xtra kuwa bado kuna mengi yanakuja kutoka kwa wachezaji wao wote waliopo ndani ya timu hiyo.

“Huu ni mwanzo nina amini mashabiki watakuwa watapata burudani na raha kwa kuwa huku kuna mawaziri wanaoshughulikia suala hilo uwanjani na inaonekana.”

Acha ujumbe