STAA mpya wa Yanga, Mkongomani Maxi Nzengeli anataka kuona timu yake, ikiandika historia ya kufika mbali katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu hiyo.

Mkongomani huyo amesajiliwa na Yanga, katika msimu huu kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo, inafika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.MAXIYanga tayari imefuzu hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa kuwaondoa ASAS ya nchini Djibouti kwa jumla ya mabao 7-1.

Nzengeli alisema kuwa, atatumia uzoefu na uwezo wake alionao katika michuano hiyo ya kimataifa kuhakikisha wanafikia malengo yaliyowekwa na uongozi, mashabiki kwa pamoja katika msimu.

Maxi Nzengeli alisema kuwa, malengo ya kwanza ni kuona timu inafika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea makombe yote waliyoyachukua msimu uliopita.


“Sisi wachezaji wapya tuna deni kubwa la kulilipa hapa Yanga katika msimu huu, na la kwanza ni kuhakikisha timu inafika mbali katika Makundi Afrika.MAXI“Wachezaji wenzetu waliokuwepo msimu uliopita waliifikisha Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na sisi wapya tunatakiwa kufanya kitu kikubwa zaidi msimu huu.

“Nikiwa kama mchezaji nitahakikisha ninapambana ili niingie katika kikosi cha kwanza kwa lengo la kuisaidia timu yangu ifikie malengo kwa kuipa matokeo mazuri,” alisema Maxi Nzengeli.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa