NYOTA wakazi ndani ya kikosi cha Simba, Fabrince Ngoma, Willy Onana, Luis Miquissone na Saido Ntibanzokiza wameipa jeuri Simba kuwakabili wapinzani wao kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni Power Dynamo ya Zambia hawa wanatarajia kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa na kete ya kwanza inatarajiwa kuwa ugenini kati ya Septemba 15-17.simbaIkumbukwe kwamba timu hiyo ilicheza na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo huo ubao ulisoma Simba 2-0 Power Dynamo ni Ngoma na Onana walifunga mabao mawili kwa Simba huku Ntibanzokiza akitoa pasi zote mbili za mabao na lile la pili pasi hiyo ilianzia kwenye pigo la kona fupi iliyopigwa na Luis.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameliambia Championi Jumatano kuwa, kikubwa wanachokifanya ni maandalizi mazuri kwa kila mechi.simba“Tuna silaha nyingi za kutumia kwenye mechi za kimataifa kumbuka tuna wachezaji waliofunga kwenye mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo na wapo wale walioimarisha ukuta hivyo tunaamini tutafanya vizuri.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa