MABOSI YANGA WAISUKIA EL-MERREIKH MIKAKATI

MAKAMU wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema kuwa uongozi wao umeweka mikakati mizito ya kuhakikisha wanafanikisha malengo ya kufuzu Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Viongozi hao hivi sasa wapo katika mikakati ya kuhakikisha wanawaondoa Al Merreikh ya Sudan katika hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.yangaYanga imefanikiwa kufuzu hatua ya Kwanza ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa kuwaondoa ASAS ya nchini Djibouti kwa jumla ya mabao 7-1.

Arafat alisema kuwa, uongozi umejifunza kupitia msimu uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika kila hatua wanayofikia ya michuano ya kimataifa ushindani unaongezeka kutokana na kukutana na timu kubwa na zenye ubora.

Arafat alisema kuwa, wameliona kama uongozi utahakikisha unatimiza majukumu yake ikiwemo kuwezesha mahitaji ya timu ikiwemo kambi nzuri na bonasi kwa wachezaji.

“Tunawaondoa ASAS sio kwamba wabaya, ni timu nzuri inayocheza kitimu na kama sio ubora wa wachezaji wetu tusingefanikiwa kufuzu hatua ya Kwanza.

“Niwatake wachezaji wetu kuendelea kupambana uwanjani kwa lengo la timu ipate matokeo mazuri, kwani mbeleni tuna kibarua kigumu.yanga“Msimu uliopita tulijifunza kitu wakati tunacheza Kombe la Shirikisho Afrika, ni kuwa kadiri unavyofuzu kwenda hatua inayofuatia michuano ya kimataifa unakutana na timu bora kama ilivyokuwa Yanga, tumejipanga katika hilo,” alisema Arafat.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.