Ligi kuu ya Tanzania kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Yanga watawakaribisha JKT Tanzania kwaajili ya mchezo wao wa pili wa Ligi katika dimba la Chamazi.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1:00 usiku huku mechi ya kwanza vijana wa Gamondi waliondoka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Walipa Kodi.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Wakati kwa upande wa JKT wao pia walianza vyema kwa kupata alama tatu dhidi ya Namungo na leo hii wanahitaji alama zingine mbele ya Young Afrcans ambao wanaonekana kuwa imara zaidi.
Ikumbukwe kuwa Yanga wakishinda kwa zaidi ya mabao mawili hii leo, wataongoza Ligi kwa kuwa na mabao mengi. Na pia endapo JKT watashinda wao watashika nafasi ya 3 kwenye msimamo.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Vijana wa Jangwani ndio mabingwa watetezi wa Ligi kuu wakichukua ubingwa huo mara mbili mfululizo na msimu huu wamefanya usajili mzuri wa kutetea taji hilo tena na wanajiamini kwa hilo.