Yanga Kumenyana na EL-Merreikh Raundi ya Kwanza CAFCL

Baada ya ushindi mnono hapo jana dhidi ya Asas Djibout kwa aggregate ya (7-1) klabu ya Yanga hatimaye wamenyana dhidi ya EL-Merreikh ya Sudan katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.

 

Yanga Kumenyana na EL-Merreikh Raundi ya Kwanza CAFCL

Yanga wamefika hatua hiyo baada ya kuifunga Asas jumla ya mabao 7-1 kwenye michezo yote miwili na kumfanya asonge mbele kwenye michuano hii ambayo inafanyika kila mwaka Barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa Young Africans wao msimu uliopita walicheza kombe la shirikisho Afrika na kufanikiwa kuwa mshindi wa pili kwa kupata Medali baada ya kutolewa na USM Alger. Lakini msimu huu wapo Ligi ya Mabingwa.

Yanga Kumenyana na EL-Merreikh Raundi ya Kwanza CAFCL

Usajili ambao wameufanya unaonekana kwenda kuwalipa kutokana na kiwango ambacho wachezaji hao wanaonyesha kama vile, Max Nzengeli, Pacome, Konkoni, na wengine kibao.

Pia klabu hiyo kwasasa ina kocha mpya Gamondi ambaye amepata sifa mbalimbali kutoka kwa wachambuzi pamoja na mashabiki kuwa ana ubora mkubwa sana hivyo vijana hao wa Jangwani msimu huu Ligi ya Mabingwa watafika mbali sana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.