Hatimaye imejulikana sasa, klabu ya Simba SC itamenyana dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa msimu huu wa 2023/24.
Mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya tarehe 15, 16, na 17 Septemba ambapo Mnyama ataanzia ugenini, na mechi ya pili iatapigwa Dar es salaam kuanzia tarehe 29, 30 mpaka tarehe 01 Oktoba.
Timu hizi zilikutana kwenye mechi ya kirafiki wiki kadhaa zilipoita ambapo Simba alikuwa akiadhimisha siku yake na Power Dynamos walifungwa kwa mabao 2-0 katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Msimu uliopita Wekundu wa Msimbazi aliishia hatau ya robo fainali ya CAFCL kwa kutolewa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya penati akiwa kule Mohamed V Morocco baada ya timu hizi kila mtu kushinda kwake.
Sasa timu imeleta wachezaji wapya kikosini ambao wanatarajiwa kuongeza kitu klabuni hapo na kuwasaidia kufika mbali kwenye michuano hii ikiwemo kufika Nusu Fainali mpaka Fainali yenyewe na kubeba Ubingwa.