Inaelezwa kuwa kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kimeeleweka baada ya kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa miaka miwili na Mzamiru Yassin.
Habari zinaeleza kuwa uongozi wa Simba umeamua kufanya naye mazungumzo mapema kabla mambo hayajawa mengi kwa kuwa kuna timu ambazo zinahitaji saini ya kiungo huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Mzamiru ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Juma Mgunda kwenye mchezo dhidi ya KMC walipopata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Saido Ntibanzokiza alianza kikosi cha kwanza.
Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 29 kete yake ya mwisho kukamilisha mzunguko wa pili inatarajiwa kuchezwa Mei 28 itakuwa dhidi ya JKT Tanzania.
Mkataba wa Mzamiru ulikuwa unatarajiwa kugota mwisho mwishoni mwa msimu wa 2023/24 hivyo kikubwa ilikuwa ni baadhi ya vipengele kufanyiwa maboresho ndani ya timu hiyo na kilichobaki kwa sasa ni taarifa rasmi kutoka Simba.
Hivi karibuni Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa wanatambua kuna wachezaji watakaoondoka ndani ya timu na wale ambao watabaki.
“Kuna wachezaji ambao wataondoka ndani ya timu na wapo watakaobaki hivyo jambo la msingi ni kuwa na subira kwa kuwa kila kitu kitakuwa wazi.”