Mechi nyingine ya Ligi kuu ya Tanzania ni kati ya Simba ya Robertino dhidi ya Dodoma Jiji majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Uhuru Dar es salaam.
Hii ni mechi ya pili kwa kila timu huku timu zote mbili zikiwa zimetoka kupata ushindi mechi zao za kwanza za ligi ambapo mnyama alishinda ugenini dhidi ya Mtibwa na Dodoma alipata ushindi kutoka kwa Coastal Union.
Simba inahitaji pointi tatu ili kutetea taji la ligi kuu ambalo wamelikosa kwa mara ya pili mfululizo mbele ya watani wao wa jadi Young Africans.
Wakati kwa upande wa Dodoma Jiji wao pia wanahitaji ushindi huu wa leo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kwani biashara ni asubuhi jioni mahesabu, na kwenye ligi ukianza vizuri kuna nafasi kubwa ya kumaliza vizuri.
Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili Mnyama aliondoka na ushindi japokuwa ulikuwa wa tabu sana. Sasa timu hizi mbili zimefanya usajili wa wachezaji mbalimbali huku kwa upande wa walima Zabibu kukiwa na ahadi ya pesa kwa kila goli.
Nani kuondoka na ushindi hii leo? na Meridianbet wameweka ODDS KUBWA kwenye hii mechi, hivyo ingia sasa na ucheze.