Timu ya wanawake ya Simba Queens inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa  Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hii leo kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano na Mamelodi Ladies.

 

Simba Queens Kugombea Mshindi wa 3 Leo

Simba Queens ambayo imekuwa ni timu pekee hapa Tanzania kwa upande wa wanaume na wanawake kufika hatua hiyo, waliondolewa na Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Mamelodi, katika dakika za mwishoni za mchezo licha ya kucheza vizuri kipindi cha kwanza.

Baada ya kutolewa hatua hiyo sasa anatafutwa mshindi wa tatu ambapo Msimbazi watakipiga dhidi ya Bayelsa Queens ambao wao walitolewa na ASFAR ya Morocco ambao ndio watacheza Fainali dhidi ya Sundowns.

Simba Queens Kugombea Mshindi wa 3 Leo

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 4:00 usiku katika uwanja wa Prince Moulay Al Hassan na matumaini yapo kwa wachezaji kufanya vizuri kwenye mchezo huo ili waondoke na ushindi.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa