Klabu ya Simba tayari imeanza safari ya kuelekea Uturuki kwaajili ya kuweka kambi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi kuu ya NBC.

Simba imeanza safari hii masaa machache yaliyopita wakiwa pamoja na kocha wao mkuu Robertinho ambaye alikuwa kwao kwaajili ya mapumziko baada ya Ligi kumalizika wakiwa wametoka kapa.
Pia mnyama mpaka sasa wamefanya usajili kwa baadhi ya wachezaji kama vile kina Onana, Che Malone Fondoh, Aubin Kramo pamoja na kumrudisha David Kameta ambaye alikuwa akiichezea klabu hiyo.
Hivyo Kameta ataenda kuungana na beki wenzake kina Shomari Kapombe pamoja na Israel Mwenda katika eneo la kulia.

Huku ukiendelea kusubiri Ligi zirejee Meridianbet wanakwambia cheza michezo ya kasino ya mtandaoni, pia bashiri mechi ambazo zinaendelea Duniani ili ujiweke kwenye nafasi ya kuwa Bingwa.
Mnyama baada ya kutoka kapa msimu huu, sasa kupitia msemaji wao Ahmed Ally wanasema kuwa wanataka makombe yote msimu ujao wakianzia na Ngao ya Jamii. Je msimu ujao utakuwaje kwa mnyama?

