Klabu ya Simba imesafiri leo kuifuata Singida Big Stars kwaajili ya mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumatano katika uwanja wa Liti majira ya saa 10:00 jioni.

 

Simba Yaifuata Singida Big Stars

Simba ambayo ipo chini ya kocha mkuu Juma Mgunda itasafiri kwenda Singida kupitia Dodoma. Timu hiyo ipo nafasi ya pili, baada ya kucheza michezo 8, imeshinda mitano, sare mbili na imepoteza mchezo mmoja pekee wakiwa wamejikusanyia pointi 17 mpaka sasa.


Singida nao wapo nafasi ya 4, baada ya kucheza michezo 9 wameshinda michezo mitano, sare mbili na wamepoteza michezo miwili tu huku wakiwa na pointi 17 sawa na Simba japokuwa wao wamezidi mchezo mmoja.

Simba Yaifuata Singida Big Stars

Kila timu imejiandaa kufanya vizuri ambapo kwa upande wa Msimbazi wao wanahitaji pointi tatu muhimu ili waweze kupunguza pengo lililopo kati yao na vinara wa ligi Yanga, lakini pia kutetea taji hilo.

Walima alizeti wao wanataka pointi hizo ili wazidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya Ligi huku baadhi ya wachezaji waliokuwa Msimbazi watacheza dhidi ya timu yao akiwemo Meddie Kagere.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa