Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo timu ya Singida Big Stars itakuwa nyumbani kwake kumenyana dhidi ya Mtibwa Sugar majira ya saa 10:00 jioni.
Singida wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi zao 23, na kushinda michezo yao 13, sare tano, na kupoteza mechi zao tano, wakati kwa upande wa Mtibwa Sugar wao wameshinda mechi zao saba, sare nane na ushindi mara nane.
Mechi iliyopita Singida wameambulia pointi moja, wakati kwa upande wa walima miwa wao wamepata pointi zote tatu kwenye mechi yao iliyopita na leo wanahitaji pointi tatu muhimu.
Mechi iliyopita timu hizi zilipokutana, Mtibwa aliibuka na ushindi. Je leo hii Walima alizeti watalipiza kisasi?