Klabu ya Namungo FC kutoka mkoani Lindi, imeicharaza Geita Gold ya Minziro mabao 2-1 kwenye mchezo ambao ulipigwa hapo jana majira ya saa 1:00 usiku katika dimba la Majaliwa.

 

Namungo Yailaza Geita Gold ya Minziro

Mabao hayo kwa upande wa Namungo yalitupiwa kimyani na Lusajo pamoja na Paterne huku kwa upande wa wachimba dhahabu bao lao la kufutia machozi likifungwa na Maguli dakika ya 64.


Baada ya ushindi huo Wauaji wa Kusini wanashikilia nafasi ya 7 kwene msimamo wakiwa na pointi zao 32, huku Minziro na vijana wake wakiwa nafasi ya tano na pointi zao 34, huku tofauti ya alama kati yao ikiwa ni mbili pekee.

Namungo Yailaza Geita Gold ya Minziro

Baada ya mchezo huo, Namungo watamualika TZ Prisons kwenye mchezo wao ujao huku wachimba dhahabu wao watakipiga dhidi ya vinara wa ligi Yanga tarehe 12 mwezi Machi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa