Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili wa funga kazi unatarajiwa kupigwa leo Mei 28, 2024 kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.
Ipo wazi bingwa wa ligi ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi hesabu ni kwenye tuzo ya kiatu bora na nani atamaliza nafasi ya pili msimu wa 2023/24.
Mechi za mwisho za ligi ni maamuzi kwa kuwa tofauti ya Simba na Azam ni kwenye mabao ya kufunga ambapo mtaji wa Azam FC ni kwenye safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi na ukuta haujaruhusu mabao mengi.
Hii hapa ratiba ya mzunguko wa pili raundi ya 30 upo namna hii:-
Simba dhidi ya JKT Tanzania
Geita Gold dhidi ya Azam FC
Yanga dhidi ya Tanzania Prisons
Namungo dhidi ya Tabora United
Coastal Union dhidi ya KMC
Ihefu dhidi ya Mtibwa Sugar
Singida Fountain Gate dhidi ya Kagera Sugar