Uongozi wa Klabu ya Yanga umeomba Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), kuhamishia mechi zao mbili za ligi Jijini Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Yanga wameomba jambo hili ili kufanya ya Kihistoria ya kusherehekea Ubingwa wao wa 30 Kwa Parade la treni ya mwendokasi kutoka Dodoma hadi Dar Es Salaam kama watakubaliwa.
Licha ya kuomba michezo yao ya mwisho kucheza Dodoma lakini pia wana mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao utafanyika CCM Jamhuri Mei 22.
Yanga Baada ya kumalizana na Dodoma kesho kutwa, watakuwa na michezo miwili wakiwa nyumbani, Mei 25 watacheza dhidi ya Tabora United na Mei 28 dhidi ya Tanzania Prison.
Hivyo wanataka mechi zote wacheze Dodoma na kuna uwezekano mkubwa wa ombi lao kukubaliwa.