JUMA MGUNDA NA HESABU ZA KIKABE LIGI KUU

Juma Mgunda Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho kinahitajika katika mechi zilizobaki ni kupata matokeo mazuri.

JUMA MGUNDA NA HESABU ZA KIKABE LIGI KUU

Ni hesabu ndefu kwa Mgunda kupambaniakupambania nafasi ya pili dhidi ya Azam FC zote zikiwa na pointi 60 kibindoni baada ya kucheza mechi 27 msimu wa 2023/242023/24.

Mchezo uliopita wa ligi Simba ilipata pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji ambapo mwamba Saido Ntibanzokiza alirejea kikosi cha kwanza baada ya kukosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.

Ipo wazi kwambakwamba katika mchezo huo bao la ushindi lilifungwa na Michael Fred dakika ya 7 akifikisha mabao 6 ndani ya ligi msimu wa 2923/24.

JUMA MGUNDA NA HESABU ZA KIKABE LIGI KUU

Mgunda amesema: “Ambacho tunahitajitunahitaji ni kupata matokeo mazuri kwenye mechi hilo lipo wazi ninawapongeza wachezaji kwa kuwa wanajituma na kutimiza majukumu yao.
“Makosa katika mechi zetu tunayafanyia kazi na mazuri tunayachukua kwa ajili ya kuwa imara katika mechi zilizobaki mbele yetu.”

Katika Mzizima Dabi Uwanja wa Mkapa ilikuwa Azam FC 0-3 Simba mabao yakifungwa na Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma na Duchu.

Bingwa wa ligi ni Yanga mwenye pointi 71 baada ya mechi 27 hazitafikiwa na timu yoyote Bongo.

Acha ujumbe