Klabu ya Yanga inatarajia kushuka Dimbani hii leo kumenyana dhidi ya Singida Big Stars kuwania kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda mchezo wake uliopita.

 

Yanga na Singida Kuwania Nusu Fainali Leo

Yanga baada ya msimu uliopita kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano hii, msimu huu amepania kuondoka na kombe hilo huku akiwa bado ni kinara wa Ligi hadi sasa akiwa amepoteza mechi moja pekee.

Lakini pia Singida nao wanahitaji ushindi ili waweze kuingia hatua inayofuata na ikiwezekana wacheze na fainali kabisa kwa mara ya kwanza baada ya kupanda daraja msimu huu huku wakiwa na mwendelezo mzuri wa matokeo.

Yanga na Singida Kuwania Nusu Fainali Leo

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya 2:15 usiku huku mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, walikutana kwenye ligi na Singida alipoteza kwa mabao 4-1. Je hii leo Walima alizeti wanaweza kulipiza kisasi ikiwa Young Africans wamefanya mchanganyiko wa kikosi?

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa