Mudathir Yahaya Atambulishwa Yanga

Klabu ya Yanga imemtambulisha kiungo wa zamani wa klabu ya Azam Fc Mudathir Yahaya kama mchezaji wao mpya ndani ya klabu hiyo kama usajili wa kwanza wa dirisha dogo mwezi Januari.

Baada ya kufanikiwa kutangaza kumuongezea mkataba golikipa wake namba moja siku ya jana Djigui Diarra, Leo imefanikiwa kumtangaza kiungo huyo ambaye aliachana na klabu ya Azam tangu mwanzoni mwa msimu huu.mudathir yahayaKiungo huyo ambaye amekua na uzoefu mkubwa katika ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa ameitumikia klabu ya Azam kwa muda mrefu sana na kwa kiwango kikubwa pamoja na klabu ya Singida United, Hivo ni wazi ni mchezaji mzoefu ambaye ataongeza kitu kwenye klabu hiyo.

Timu ya Yanga ipo kwenye mipango ya kuimarisha kikosi chake kwajili ya kupambana kwenye michuano ya kimataifa, Huku pia wakitaka kutetea mataji yake ya ligu kuu ya NBC pamoja na taji la kombe la Azam Federation ambao ni mabingwa watetezi.mudathir yahayaMudathir Yahaya aanakwenda klabu hiyo kwajili ya kuimarisha eneo la kiungo ambalo limeondokewa na moja ya wachezaji wake bora kabisa kwenye eneo hilo Feisal Salum, Kuongozeka kwa kiungo huyo kutaimarisha kwa kiasi kikubwa eneo la katikati kwenye timu hiyo kwani ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa pamoja na uzoefu wa kutosha.

 

Acha ujumbe