Ofisa Habari wa klabu ya Azam, Thabit Zacharia, amesema wamekubali matokeo ya mechi ya nusu Fainali ya kombe la FA na yamewaumiza, lakini wanakwenda kujipanga kulipiza kisasi kwenye uwanja wao wa nyumbani mchezo wa Ligi Kuu.
“Tumekubali kufungwa. Tulipoteza umakini tukafungwa goli mwishoni. Pamoja na hayo tulikuwa na uwezo wa kuimaliza mechi mapema.
“Kuna nafasi ambazo wachezaji wetu walizipata, Salum Aboubakar, Idd Nado na Mudathir Yahaya, walipata nafasi ambazo zingeweza kumaliza mchezo, lakini hatukuzitumia.
“Tumerudi nyumbani kujipanga na mechi nyingine dhidi ya Simba Julai 14 kwenye Uwanja wetu, Chamazi, nina uhakika tutalipa kisasi.
“Itakuwa ni mechi ya kisasi. Pia tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri,” alisema ofisa habari huyo wa Azam.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

