Karia Hana Mpinzani Kwenye Urais TFF

Wallace Karia anakuwa mgombea pekee wa nafasi ya Kamati ya Urais wa TFF baada ya wagombea wengine wawili [Hawa Mniga na Evance Mgeusa] kukosa sifa za kuendelea na uchaguzi kwa hatua inayofuata.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Benjamin Kalume amesema, Karia anasubiri kuthibitishwa na Mkutano Mkuu lakini si kupigiwa kura.

Karia ambaye amekuwa chachu ya mabadiliko mengi kwenye sehemu ya mpira wa Tanzania amebaki mwenyewe kwenye nafasi hiyo baada ya wenzake wawili kuondolewa kutokana na kutokidhi vigezo ambavyo havijatajwa.

Miongoni mwa mambo kadhaa aliyoyafanya rais huyu wa TFF ni kutengeneza mazingira mazuri ya soka nchini kote kwa upande wa klabu zinazoshiriki ligi kuu na hata katika timu ya taifa.

Kwa upande wa vilabu, hivi karibuni TFF chini ya rais huyu ilifanikiwa kusaini mkataba wa udhamini wa matangazo na Azam Media wenye thamani zaidi ya bilioni 225.6 kwa miaka 10.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.