Allegri: Pogba Kurejea Hivi Karibuni

Kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri amesema kiungo wake Paul Pogba amekaribia kurejea kwenye timu hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye amejiunga na klabu ya Juventus kwenye dirisha kubwa la majira ya joto, Mpaka sasa hajafanikiwa kucheza mchezo wowote wa mashindano ndani ya klabu hiyo kutokana na majeraha yanayomkabili.allegriKocha Allegri amesema  kiungo huyo anaendelea vizuri kwasasa na jeraha la goti kwasasa halimsumbui, Kwani anaweza kukimbia na kama ataendelea hivo kwa siku 15-20 anaweza kuingia kwenye timu amesema kocha huyo.

Pogba amekua akisumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu ambayo yamekua yakimuweka nje mara kwa mara, Na hii imetokea pia ndani ya klabu ya Manchester United ambapo pia alikua akisumbuliwa na jeraha la goti lililokua linamueka nje ya uwanja kwa muda mrefu.allegriMassimiliano Allegri ametoa taarifa juu ya kurejea kwa kiungo wake huyo ambaye amekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Lakini kocha huyo hajaeleza tarehe rasmi ni lini kiungo huyo atarejea na kuanza kuitumikia miamba hiyo ya Turin klabu ya Juventus.

Acha ujumbe