Liverpool wanaripotiwa kutaka kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kumsajili mshambuliaji wa Wolves Matheus Nunes.

Liverpool walianza vibaya msimu wa 2023 baada ya kufungwa 3-1 ugenini Brentford jana usiku kwenye mchezo ambao walikuwa wakiongozwa mara kwa mara katikati mwa uwanja.
Jurgen Klopp alikuwa akimtaka nyota wa Kimataifa wa Ureno Nunes katika majira ya joto kabla ya kujiunga na Wolves kwa kitita cha pauni milioni 38.
Na sasa miezi mitano tu baadaye, gazeti la The Telegraph linasema watafanya jaribio jingine la kumnasa hadi Anfield katika dili ambalo lingegharimu pauni milioni 44. Akiwa na kiwango cha juu alipofika kutoka Sporting Lisbon, mchezaji huyo ameanza michezo 12 kati ya 14 ya ligi ya daraja la kwanza ya Wolves msimu huu.

Imeelezwa kuwa kama Liverpool wataweza kufanya makubaliano na klabu hiyo ya West Midlands, Nunes atajiunga na majira ya joto badala ya kufanya mabadiliko ya katikati ya msimu.
Vilabu hivyo viwili vilijadiliana kwa amani wakati Diogo Jota alipohamia Merseyside mwaka 2020, wakati wakala wa Nunes Jorge Mendes alihusika katika mazungumzo ambayo yalimfanya Darwin Nunez kusajiliwa kutoka Benfica msimu uliopita wa joto.

Na Liverpool wanaamini kuwa Nunes mwenye mechi 11 ni mchezaji mwingine ambaye anaweza kuwa na mustakabali mkubwa Anfield.

