Ihefu Kumualika KMC Hii Leo

Ligi kuu ya NBC inaendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Ihefu ya Mbeya watakuwa wenyeji wa KMC katika mchezo wao wa raundi ya 19 majira ya saa 10:00 jioni.

 

Mchezo huo wa Ihefu na KMC utapigwa katika uwanja wa Highland Estate huku kila timu ikihitaji ushindi wa pointi 3 ili iwezo kupanda nafasi inayofuata kwani huu ni mzungukko wa pili.

Ihefu wapo nafasi ya 13 baada ya kuchezo 18 na kufanikiwa kushinda mechi tano, sare mbili na kupoteza michezo 11 na kujikusanyia pointi zao 17 ambazo bado sio salama kwao.

KMC wao baada ya hiyo michezo 18 waliyocheza wameshinda michezo yao mitano wakaenda sare saba kupoteza mara sita na alama 22 huku wakiwa nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi.

Mechi iliyopita walipokutana, KMC aliondoka na pointi 3. Je hii leo mwenyeji atakubali kudondosha alama akiwa nyumbani kwake?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.