Klabu ya Al Ahly wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Confederation of African Football (CAF ) Super Cup baada ya kuwafunga Raja Casablanca kwa mikwaju ya penati.

Fainali hiyo iliyopigwa nchini Qatar ilishuhudia mabingwa hao watetezi wa kombe hilo wakitoka sare ya magoli 1-1 katika dakika tisini kabla ya kushinda kwa penati 6-5.
Al Ahly wameingia katika fainali hizo baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya 10 wakati Raja Casablanca akiingia katika fainali hizo baada ya kutwaa kombe la shirikisho barani Afrika.
“Ninawashukuru wachezaji wangu, benchi la ufundi na mashabiki, ” alisema meneja wa Al Ahly, Pitso Mosimane. “Tulifanya mazoezi ya penati na tumefanya vile jinsi tulivyofanyia mazoezi.
“Ilikuwa ni ngumulakini tulifikiri itakuwa hivi. Raja walicheza kupoteza muda lakini sisi ni Al Ahly na tuna spiriti.” aliongeza.
Mabingwa hao wa CAF Super Cup wana nafasi nyingine ya kutwaa taji msimu huu pale watakapocheza katika michuano ya FIFA Club World Cup mwezi wa pili mwaka ujao.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


