Arteta Anatarajia Saka Kupona Kabla ya Kombe la Dunia

Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa jeraha la Bukayo Saka ni pigo tuu kwao na haliwezi kumuondoa katika kucheza Kombe la Dunia na Uingereza linalotarajiwa kupigwa Qatar mwezi ujao.

 

Arteta Anatarajia Saka Kupona Kabla ya Kombe la Dunia

Arsenal waliibamiza Nottingham Forest kwa mabao 5-0 na kupanda hadi kileleni kwa Ligi kuu ya Uingereza wakiwa na pointi 31 ambapo Saka alitoa assist yake ya 20 ndani ya EPL huku Martinelli akiiandikia The Gunners bao la kwanza dakika ya tano ya mchezo.

Huku assist hizo zikifanywa na Cesc Fabregas na Wayne Rooney pekee wakiwa katika umri mdogo kuliko mchezaji huyo wakiwa na umri wa miaka 21. Arteta anasema kuwa mchezaji huyo alilazimika kutoka nje dakika ya 27 kutokana na kile kilichoonekana kuwa jeraha lakifundo cha mguu wa kushoto kufuatia mpira uliopigwa na beki wa kushoto wa Nottingham Forest, Renan Lodi.

Arteta Anatarajia Saka Kupona Kabla ya Kombe la Dunia

Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate alikuwa na wasiwasi kwamba Saka angejiunga na wachezaji wenzake kama Kalvin Phillips na Kyle Walker kwenye orodha yake ya majeruhi, ingawa kocha wa Arsenal Arteta anaamini winga huyo atakuwa sawa.

Lakini pia alipoulizwa kama Bukayo anaweza kukosa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia akiwa na Uingereza dhidi ya Iran mnamo Novemba 21, Arteta alisema anatumaini atakuwepo japokuwa aliumia vibaya akitoka uwanjani anachechemea.

Arteta Anatarajia Saka Kupona Kabla ya Kombe la Dunia

Arteta na vijana wake msimu huu wapo na uimara mkubwa sana huku wakilenga kubeba ubingwa wa Uingereza ambao wameukosa kwa muda mrefu na mechi ijayo watakuwa uwanjani kukipiga dhidi ya Chelsea ambapo ni Dabi ya London.

Acha ujumbe