Okrah Awashukuru Mashabiki kwa Kumkosoa

WINGA wa Simba SC mwenye kasi na ujuzi wa kukaa na mpira ambaye pia ni raia wa nchini Ghana, Agustine Okrah ametumia mtandao wake wa kijamii kuwashukuru mashabiki zake kwa kumkosoa kutokana na makosa aliyokuwa akiwayafanya kwenye michezo iliyopita.

 

Okrah Awashukuru Mashabiki kwa Kumkosoa

Okrah Magic, katika mchezo wa jana aliisaidia timu yake ya Simba kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiwa pia alihusika kwenye goli la kwanza lililofungwa na Mzamiru Yassin kabla ya kufunga bao 3 kwenye kipindi cha pili.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Okrah aliandika ujumbe maalum kwa mashabiki zake.

“Asante kwa ukosoaji na kunitia moyo kwa siku chache. Nimefurahi tumerudi kwenye njia ya ushindi. Ninajifunza kuishi, ili kuacha alama kwenye bustani. Tutafanikiwa.”

 

Okrah Awashukuru Mashabiki kwa Kumkosoa

Mchezaji huyo alianza kukosolewa kwenye mechi ya dabi dhidi ya Yanga SC, baada ya kushindwa kutumia nafasi zilizokuwa na uwezekano wa kuwa magoli, lakini kutokana na kile kilichotafsiriwa na wengi kuwa ni Ubinafsi aliandika pia baada ya mechi hiyo kuwa “Kila kitu nachofanya huwa naifikiria timu kwanza”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.